Miale ya jua ilimulika ikipiga mapaa kutokea upande wa magharibi kuashiria machweo yalikuwa yakichukua nafasi weakati huo.Sauti za watoto wakicheza nje ya nyumba zao ziliongeza uhai wa eneo lile, mbuzi nao walikuwa wakirudishwa mabandani mwao na wamiliki ama vibarua waliokuwa wameletw akuishi pale kwa ajili ya kazi hiyo.
Nyasi za kijani kibichi pamoja na majani ya kiti mirefu ya kupandwa yalikuwa yakipelekeshwa na upepo huku na kule kadiri ulivyotaka .
Sauti za matairi ya magari yaliyokuwa yakisugua barabara ya lami zilisikika kutoka mbali huku sauti zikerazo za pikipiki zikisikika kama vile zikishindana na na sauti za ngurumo za magari makubwa.Honi za pikipiki na taksi zilisikika si kutaka kupishwa bali kusaka abiria ambao wengi walikuwa wakitoka kazini na wachache walikuwa wakiiingia kazini.
Kina mama na mabinti zao walisikika wakipepeta mchele na kuagizana vibandani kununua viungo ambavyo ama havikununuliwa ama havikutosha , huku akina baba nao wakiwa na vijana wao wa kiume wakimwagilia bustani na kuchuma mboga za majani ambazo walipenda kudai kuwa walikuwa wakizipalilia kw akupunguza majani yaliyokuwa yamezidi.
Wakati hayo yakiendelea, ndani ya nyumba moja kuna kijana alikuwa amekaa tuu akisikiliza muziki ambao hata baada ya umeme kukata na redio kuzima aliusikia ule muziki huku akiimba kwa kumung’unya maneno ambayo hakuyakumbuka. Mwalimu Godwin Joseph alikuwa akiendelea kuimba nyimbo za msanii wa Bongo Fleva Sam wa ukweli ambazo alikuwa akizisikiliza kabla ya umeme kukata bila kujua kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa akigonga mlango wa nyumba yake kwa muda mrefu hadi aipochukua uamzi wa kuingia pale ndani.
‘’Shikamoo mwalimu’’Alisalimia Kurwa mwanafunzi wake shuleni Njombe sekondari ambaye kwa kipindi hicho alikuwa likizo.
‘’ Mhh-m-maa-Marhhabaa vipi umegonga sana?’’Alibabaika Godwin akisugua macho yake yalikuwa makubwa kama ma apple ya Uwemba kwa viganja vyake vilivyonyimwa nyama za kutosha kushikilia viunzi .
‘’Ndiyo mwalimu Sikai sana kuna barua yako amenipa mkuu amesema ilitumwa kwa anuani ya shule’’Aliongea Kurwa akimpa barua iliyokuwa imewekwa kwenya bahasha iliyovutia kwa rangi na urembo wake.
‘’Asante sana karibu Soda ipo kwenye jokofu fungua hapo jihudumie’’Aliongea Godwin akielekeza kidole kwenye jokofu lililokuwa limejee pombe nyingi ingawa hakuwa mnywaji wa pombe alipenda sana kuwawekea rafiki zake ambao wengi walikuwa wakipenda kunywa pombe.Alikuwa amejaribu kunywa pombe zaidi ya mara nne lakini aliishia kutapika na kupata homa hivyo akaamua kuachana nayo zadi ya kuzitazama kwenye ndani ya jokofu lake.
‘’Asante mwalimu kuna mtu nilikuwa na miadi naye namuwahi’’Alijibu Kurwa akifungua mlango na kutaka kutoka.
‘’Vipi shem nini? Maana watoto wa uzunguni ukiwakosa wakiwa na nafasi basi utasubiri mwaka tena unakuja kumwona na mshikaji mwingine wahi bhana’’Aliongea Mwalimu Godwin akicheka.
‘’Hapana mwalimu , baadaye nitakuja tuongee’’Kurwa akiongea akiwa nje ya ile nyumba.Alimzoea mwalimu wake wa Geography ambaye alikuwa ni kama rafiki yake tuu lakini alikuwa akimficha sana juu ya masuala ya mahusiano kwani licha ya mwalimu wake kupenda sana nyimbo na tamthilia za mapenzi hakuwahi kumwona akiwa na mpenzi wala kusikia akimwongelea, alijua labda kwa kuwa aikuwa akimwona kama mwanafunzi hivyo aliamua kumficha.Kauli ya kumwambia kuhusu wasichana wa uzunguni ni kweli wana tabia kama zile , je miezi tisa aliyokaa Njombe ilitosha kuzijua tabia zao bila kujihusisha nao?. Hayo ni baadhi ya mambo aliyokuwa ametoka nayo Kurwa kwa mwalimu wake ‘’msela’’ kama alivyokuwa akiiitwa na wanafunzi wake bila kujua.
Mwalimu Godwin alijikuta akipata kigugumizi kuifungua ile barua ambayo kwa mwonekano wake ilikuwa ikionesha kabisa ni suala la mapenzi lilikuwa ndani mwake lakini ni nani ambaye alikuwa ameiandika, kwa nini atumie anuani ya shule?, kwa nini aandike barua badala ya kumpigia simu? Hakuifungua ile bahasha nzuri ambayo kuifungua tuu kungekuwa kama kuharibu nakshi zake zaidi ya kuigeuza geuza pengie jina la mwandishi wa barua lingeandikwa nyuma ya ile barua lakini hakuona chochote zaidi ya nakshi za’ I Love You’ zilizokuwa na maua ya kuchorwa na kubandikwa.
Mra simu yake ilionesha kuwa palikuwa na ujumbe uliokuwa umeingia akawahi kama kibaka akikwapua mkoba wa ‘ Sister Duu’ na kufungua ujumbe ambao akili mwake alijua utakuwa umetoka kwa mtu ambaye ana wiki mbili hapatikani simuni alitamani kupata ujumbe wake.Alitamani kusikia kilichomfanya asipatikane , alikumbuka kuwa mara ya mwisho kuongea naye walibishana juu ya jambo fulani na simu ilipokatwa na huyo mtu haikupatikana tena.
‘’NDUGU MTEJA KIFUSHI CHAKO CHA CHEKA KIMEKWISHA, SASA UNAWEZA KUONGEA BURE BAADA YA DAKIKA TATU ZA KWANZA, asANTE KWA KUTUMIA VODACOM’’
Ulisomeka ule ujumbe na kumfanya asonye kwa sauti , hakutegemea kukutana na ujumbe ule aliouita wa kipumbavu kwani kila muda ule ulikuwa ukiingia simuni mwake na alijiunga tena na huduma ile kwa matarajio ya kumpata mtu ambaye wiki ya pili alikuwa akimtafuta simuni bila mafanikio.
Akiwa na na hasira juu ya ule ujumbe simu ujumbe mwingine uliiingia na haraka haraka akaufungua na kukutana na kitu ambacho pia kilimkera.
‘’NMB INAKUKUMBUSHA KUHAKIKISHA TAARIFA ZAKO ZA BENKI KABLA YA MWAKA KUISHA KUEPUKA USUMBUFU WA KUFUNGIWA AKAUNTI YAKO’’ TUNAKUTAKIA SIKUKUU NJEMA YA X-MASS NA MWAKAMPYA’’
Baada ya kuusoma ujumbe huu wa pili ulimkera ukampa mwanga fulani juu ya ile barua aliyokuwa ameipokea alijua lazima itakuwa ni kadi kwa ajili ya kumtakia sikuu njema , lakini hakuweza kutabiri aliyekuwa amemtumia kadi hiyo.
Aliifungua ile bahasha kwa umakini mkubwa, lakini ujumbe mwingine uliingia simuni , huku akisonya sonya alifungua tena ujumbe ule huku akitegemea kitu ambacho kisingemkera lakini baada ya kusoma alijikuta akiongea mwenyewe.
‘’Haya mameseji yao ya kudownload yananiboa’’alifuta ule ujumbe bila hata ya kumaliza kusoma , ulikuwa ukihusu kuisha kwa mwaka na kuanza kwa mwaka mwingine.
Akairudia tena bahasha na kuifungua yote ambapo aikutana na picha ya mtu aliyekuwa akiisubiri simu na meseji yake kwa takribani wiki mbili na barua ambayo aliifungua kwa pupa kama mtoto afunguavyo zawadi iliyofungwa kwenye boksi.
CHUO KIKUU CHA MWENGE
S.L,P 2676,
MOSHI.
17/012/2014